Wednesday, March 12, 2014

                                                        Baadhi ya vitu tulivyonunua

Tulipofika wengine tulikaa chini na wengine kwenye kitanda kilichokuwepo sebuleni
                                    
Huku tukisaidiana na majirani waliokuwepo karibu kila mama alibeba alichoweza kwa namna yake
tulishuka vilima na mabonde kuelekea kwenye Furaha Children's Home Centre

tulinunua vifaa kwaajili ya matumizi ya watoto wetu shughuli ilikuwa kuvifikisha mana gari iliishia umbali wa kama mt.150 hivi. na njia ya kufika kwenye nyumba ni vilima na mabonde. picha ya juu mwenye kikoi ni mwenyeji wetu Suzy, ambaye ndo mlezi wa watoto. wenye sare ni akinamama wa HELAU wakishusha mizigo kwenye gari
Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani jamani yaweza kufanywa kwa namna tofauti, kwa Mfano wana HELAU waliadhimisha kama ifuatavyo:

Tulijipanga, na kwa msaada wa Afisa Maendeleo ya jamii kata ya Mbezi Juu tulikifahamu kituo cha watoto Yatima kilichopo ndani ya Kata yetu kinachoitwa Furaha Children's Home Centre.

Hapo ndipo tulipofanyia maadhimisho ya tarehe 8/03 /2014 (siku ya wanawake Duniani,
Tukiwa kama wanawake wenye Hekima tuliwakumbuka watoto waliopo kwenye mazingira hatarishi kwa kupeleka msaada kwenye Kituo Hicho.

Haikuwa kazi ndogo kufika mahali hapo kwani njia ni mbaya na gari haikuweza kufika kwenye nyumba husika.
Fuatilia yaliyojiri;

Siku ya wanawake duniani ki Hekima zaidi

Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani jamani yaweza kufanywa kwa namna tofauti, kwa Mfano wana HELAU waliadhimisha kama ifuatavyo:

Tulijipanga, na kwa msaada wa Afisa Maendeleo ya jamii kata ya Mbezi Juu tulikifahamu kituo cha watoto Yatima kilichopo ndani ya Kata yetu kinachoitwa Furaha Children's Home Centre.

Hekima Ladies Walivyoadhimisha Siku ya wanawake Duniani