Tuesday, March 27, 2018

HEKIMA LADIES WALIVYOADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MWAKA 2018

''Hekima ni halibora ya mtu katika kutambua ukweli wa binadamu, vitu, matukio na mazingira mbalimbali hata kuchagua vizuri jambo la kufanya''(Chanzo Wikipedia)

hii ndio maana hawa wanawake wenye hekima walichagua vizuri namna ya kuiadhimisha siku ya wanawake ya mwaka 2018, siku ya wanawake ambayo ni tarehe 8 March kila mwaka, mwaka huu iliangukia Alhamis, kwa hekima walizonazo wamama hawa walichagua kuadhimisha siku hiyo kama kikundi mwisho wa wiki yaani jmosi tarehe 10March, ili waweze kujiunga na wanawake wengine siku ya Alhamis ktk kuadhimisha siku hii muhimu kwao. fuatilia matukio hapo chini;


tuliongozwa na Katibu wetu Vesca Lwenje, kushoto na tulipokelewa na Mwalimu mkuu wa shule ya msingi salasala mama
Ngaiza.



 Tuliketi ofisini kwa mwalimu mkuu






Mshauri wetu wa Chama Graceana Maganga alitoa historia fupi ya kikundi, na lengo la sisi kutembelea shule hii. Mwenyekiti wetu Eva Bugoye alipata dharura tunasikitika hatukuwa nae siku hii.

 Mweka hazina wetu Joyce Swai akipongezana na mwalimu mkuu baada ya kutoa ufafanuzi wa namna fedha za kikundi zinavyo patikana na zinavyotumika


Mwalimu mkuu alikuwa pamoja na msaidizi wake mwalimu William, wote walifurahia ujio wetu na walitupongeza sana kwa moyo tulionao wa kutoa msaada kwa watoto tusowajua



Mzigo wa Madaftari na Pencil HB 621 
hope kila mtu anaelewa HB pencil na MOR papers, kwa kifupi ni kwamba siku hizi mtihani wa taifa darasa la saba watoto wanatumia pencil upo hapo!


 ni furaha iliyoje tulishusha mzigo na kukabidhi,
sababu iliyotufanya tuchague shule ya msingi salasala ni katika pitapita zetu tuligundua ni miongoni mwa shule dhaifu kwenye wilaya ya kinondoni na ofisi za kikundi chetu zipo jirani na shule Charity begins at home




Mshauri wa chama  alimkabidhi Mwalimu mkuu muhtasari wa vifaa vilivyowasilishwa


 tulipata pia wasaha wa kusalimiana na watoto wachache wa madarasa mchanganyiko waliokuja kujisomea siku hiyo ya j mosi


nini kilifuata baada ya zoezi la kukabidhi vifaa , stay tuned;








Kazi na dawa, Kazi na sala!''asiyefanya kazi na asile'' baada ya kazi ya kuwasilisha mzigo kwa watoto wetu wamama hatukufanya ajizi siku ya wanawake duniani huja mara moja tu kwa mwaka
tulitafuta kiwanja tulivu na tukajiachia sawasawa, kisha tuka rudi majumbani tukiwa fresh na tayari kwa kuhudumia waume zetu na watoto
I Love HELAU kwa kweli

Monday, March 5, 2018

HEKIMA LADIES UNION (HELAU) MKUTANO MKUU WA MWAKA 2017 ULIOFANYIKA 12/01/2018

                   Muonekano wa ukumbi wetu wa mkutano pale Khana Khazana Restaurant

                                        Mweka hazina wetu Joyce Swai katika simple pose


 Joyce Pallangyo mama Nidham katika pose na Rarukia Jighe Makam Mwenyekiti


 Mwenyekiti Eva bugoye baada ya kutupatia zawadi wanachama wote,hapana chezea Mwenyekiti  wote tulipata shawl za nguvu kama aliyojitanda Regina hapo asante sana mwenyekiti wetu
barikiwa na uongezewe ulipopunguza

                                       Grace Maganga akimshuru mwenyekiti kwa zawadi

        Hivi ndivyo katibu wetu Versca Lwenje alivyopokea zawadi toka kwa mwenyekiti


                                               Pendo hagai nae alipokea ya kwake

 Baada ya zawadi toka kwa mwenyekiti pia tuli
pokea bahasha za Bonus, hapa Joyce Pallangyo akitabasamu baada ya kukabidhiwa bahasha yake na Mwenyekiti

 Regina Njoroge nay alikamata bahasha yake
 Mweka hazina Joyce Swai pamoja na pack bahasha lkn pia aliipokea ya kwake toka kwa mwenyekiti


                                  Agnella Meena na bahasha yake with a wide smile

 
 MMh kwa shukrani zetu kwa mwenyekiti ilibidi wanachama tujipigepige kumpongeza mwenyekiti, naye alikama wekundu kadhaa toka kwa wanachama wote




Theresia Masawe na Highness Mmari wasimamizi wa mambo ya kijamii katika pose la furaha


               we'l always keep our Values i.e  Truth, Courage, Unity and Positive Change


  Mwenyekiti wetu Eva Bugoye na Makamu wake Rukia Jighe wakipongezana kwa kazi yakukipeleka mbele chama chetu  mwaka mzima wa 2017


 Kutoka kushoto ni Mweka hazina wetu Joyce Swai, Eva Bugoye Mwenyekiti, Agnella Meena kwa nyuma, Grace Maganga na  Regina Njoroge tukiwa tumewasili kwenye eneo la Tukio


 Katibu Wetu Vesca Lwenje (wa kwanza kabisa mwenye dimples)ali
 fanyakazi kubwa sana kufanikisha mkutano akiwa kama mtendaji mkuu wa Chama, kwa kweli kazi yake anaimudu


 Ilifika wakati wa Maakuli, kwa kweli it was yummmyyyyy, thanks Khana Khazana Restaurant kwa Indian Cuisine ya nguvu, kwa kweli kila mtu ali enjoy
 Agnella Meena AKA Mama Cheap Car rentals or Mama Metameta Day care, Business woman la nguvu kwa mahitaji ya gari aina yoyote na wenye watoto wadogo for standard and quality daycare and baby sitting  muone huyu dada



                                Ndani ya ukumbi wa Mkutano Khana Khazana Restaurant




     Mwenyekiti Wetu Eva Bugoye aki piga selfie moja tukiwa njiani kuelekea it was so fun kwa kweli


      Grace Maganga Mshauri wetu wa Chama akitafakari jambo kabla ya kutoa hekima na ushauri


         Here is wapiganaji wetu Eva na Vesca Mwenyekiti na Katibu wetu hongereni na poleni kwa kazi nzito ya kukiendesha chama shupavu cha wanawake wenye hekima(Hekima Ladies Union)



Wednesday, March 12, 2014




                                                        Baadhi ya vitu tulivyonunua


Tulipofika wengine tulikaa chini na wengine kwenye kitanda kilichokuwepo sebuleni
                                    
                                     
Huku tukisaidiana na majirani waliokuwepo karibu kila mama alibeba alichoweza kwa namna yake
tulishuka vilima na mabonde kuelekea kwenye Furaha Children's Home Centre



tulinunua vifaa kwaajili ya matumizi ya watoto wetu shughuli ilikuwa kuvifikisha mana gari iliishia umbali wa kama mt.150 hivi. na njia ya kufika kwenye nyumba ni vilima na mabonde. picha ya juu mwenye kikoi ni mwenyeji wetu Suzy, ambaye ndo mlezi wa watoto. wenye sare ni akinamama wa HELAU wakishusha mizigo kwenye gari
Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani jamani yaweza kufanywa kwa namna tofauti, kwa Mfano wana HELAU waliadhimisha kama ifuatavyo:

Tulijipanga, na kwa msaada wa Afisa Maendeleo ya jamii kata ya Mbezi Juu tulikifahamu kituo cha watoto Yatima kilichopo ndani ya Kata yetu kinachoitwa Furaha Children's Home Centre.

Hapo ndipo tulipofanyia maadhimisho ya tarehe 8/03 /2014 (siku ya wanawake Duniani,
Tukiwa kama wanawake wenye Hekima tuliwakumbuka watoto waliopo kwenye mazingira hatarishi kwa kupeleka msaada kwenye Kituo Hicho.

Haikuwa kazi ndogo kufika mahali hapo kwani njia ni mbaya na gari haikuweza kufika kwenye nyumba husika.
Fuatilia yaliyojiri;