HELAU walitimiza miaka 3 toka waanze umoja wao, sherehe zilifanyika January12, 2013 pale Picolo Beach Hotel. Matukio makubwa yaliyokuwepo siku hiyo ni Mkutano Mkuu wa Mwaka, na Fund Raising kwa ajili ya mfuko wa kutekeleza miradi yaChama. Fuatilia matukio katika picha
Mkutano Mkuu wa Mwaka ulianza saa nne asubuhi ambapo ulifunguliwa na Mwenyekiti Bibi Graceana Maganga, kushoto kwake ni Bibi Hyness Mmari mwenyekiti msaidizi
Katibu wa HELAU Bibi Eva Bugoye kulia akiwasilisha report ya mwaka, kushoto ni msaidizi wake Bibi Vesca Karigo Lwenje akihakikisha usahihi wa minutes
Bibi Agnella Meena ni Mweka Hzina wa Chama very serious anasisitiza kitu, alishidwa hata kuvaa sare she was carrying a baby boy zilikuwa bado siku chache ajifungue lakini she managed to work for HELAU
Ma mkubwa Bibi Joyce Pallangyo mkuu wa nidhamu akichangia mada
Viongozi wakifuatilia mada, kutoka kushoto ni Hyness na Graceana
Wajumbe wakiwa kwenye Mkutano
Katibu wetu Eva akisisitiza jambo
Mwenyekiti na Msaidizi wakipokea report toka kwa Katibu na msaidizi wake
Mweka hazina Agnella pia aliwasilisha report ya fedha akiwa na msaidizi wake Bibi Joyce Swai
Mwenyekiti na Msaidizi baada ya kupokea report zote
Mwenyekiti akiweka mambo sawa kidigitali wakati mwenyekiti msaidizi akizungumza jambo
Muonekano wa Mwenyekiti wakati akifunga mkutano
Baada ya Mkutano Mkuu kuisha tulipata Lunch
Wajumbe kwenye lunchLunch, kutoka kulia ni Theresia , Herimina, na Pendo
Ulifika wakati wa tukio muhimu la Fund Raising wajumbe walibadilisha Uniform maana ilikuwa saa kumi jioni, na mkutano mkuu ulikwisha saa nane Mchana- Chezea HELAU !
Mwenyekiti alisema neno la ukaribisho kwa wageni
Mwenyekiti Msaidizi alikuwa na neno pia
Katibu pia alikuwa na neno
Mweka hazina Msaidizi alikuwa na neno pia
Mwanachama Theresia kulia akiongea na baadhi ya wageni
Mgeni Rasmi kwenye Fund raising ni mwenye suti kushoto President wa SAM and ANZAI Fiber Boat Builders Co.Ltd akiingia ukumbini huku akisindikizwa na mpambe mwenye T shirt na jeans na wana HELAU wakiwa Nyuma
Wana HELAU Kwa raha zao
Tuli dancekwa Mbwembwe
Wageni wetu wali dance kwa furaha
Mwenyekiti aliunganisha sala na kukaribisha wageni
Akikaribisha wageni
baadhi ya wageni wetu kwenye Fund raising
Tulikuwa na wageni wa jinsia na umri tofauti
Agnella Mweka hazina hakuwa nyuma katika kuhamasisha michango itoke pamoja na Tumbo, ama kweli mwanamke kujituma
Mweka hazina Msaidizi alihangaika na Microphone ili mradi tu Pledge zitoke hahahaaa Mwanamke ubunifu
Katibu wetu Eva hakuchoka kuongeza chombezo kila apioona panahitaji ili kuongeza ufanisi wa kuchangia kwa wageni
Mwenyekiti akisema neno
Mgeni rasmi alikabidhi Cheque yenye kiasi cha kutosha tu
M/hazimna msaidizi Joyce Swai akirecord mahesabu
M/kiti akisoma risala mbele ya mgeni rasmi
Katibu na msaidizi wake wakiyarudi
Vesva- aka -katibu msaidizi akimfuta jasho mgeni rasmi baadae ntawaeleza siri ya yeye kumfuta jasho baba huyu
Mgeni rasmi akitoa Speech
Da Mercy akitoa pledge yake, da Mercy pia ni Mshauri wa wana HELAU
Engeneer Norah naye alikuwa mgeni wetu
Da Conish ni Rafiki na dada wa wana HELAU yeye alitoa Cash
Palikuwepo na zawadi kwa wanachama Wote. tulipata Vikapu vya kubebea Documents
Ni zamu ya Vesca kukabidhiwa zawadi ngoja tu ni waambieni ile sir ya vesca kumfuta jasho baba huyu. Jamani Mgeni rasmi ni mume wa Vesca!! tazama Pozi la Vesca anapotaka kupokea zawadi mwanamke pozi bwana
Nasi wana HELAU pia tulimpatia Mgeni rasmi zawadi - Di Jiwe la kung'aa mithili ya diamond (Crystal) lenye maandishi ya shukrani kwake. zawadi ilikabidhiwa na mwenyekiti kwa niaba yetu
Mgeni rasmi wetu akionesha zawadi yake - alifurahi sana - aliipenda - alikiri hakutegemea alidhani atapewa shati la batic, hahahaaaa! jamani wanawake tuwe wabunifu jamani
ulifika wakati wa maakuli jamani siri nyingine pia yule mpambe aliyeingia na mgeni rami ni mume wa Mwenyekiti wetu hapa mwenyekiti na mume wake wakipakua. kwa kifupi wana HELAU wote waliwaalika waume zao kuja kuchangia mfuko wa HELAU
kutoka kushoto wanaoonekana sura ni Mume wa katibu wetu( Eva), Eva, na joyce Swai
Mweka hazina msaidizi Joyce Swai akisoma report ya makusanyo(Pledges na Cash)
Ulifuata wasaa wa kukata cake ya aniversary ambapo alibeba Mwanachama mwenye umri mdogo kuliko wote ambaye ni Vesca kuileta mezani
Tulikata cake kwa Pamoja kuonesha sisi sote ni sawa na msingi wetu ni umoja
na kila mmoja alijilisha
Baadae tulikatia kwenye sahani na tuliwapatia wageni wetu kila meza iliwekwa sahani
Norah alikuwa ni mgeni wenye umri mdogo kuliko wote naye alilishwa cake na katibu wetu Eva
kuelekea mwisho wa shughuli mwenyekiti alitusuprise kwa kugawa zawadi kwa kila mwanachama hapa mama kijacho Agnella anaonekana akipokea zawadi - kila mmoja alipata zawadi ya Kidaka pochi. Kwa upendo binafsi wa Mwenyekiti
Nasi hatukuwa nyuma katika kumshukuru mwenyekiti na kumuonesha upendo na ushirikiano tulimtunzaje mwenyekiti!? chezea HELAU
Mwenyekiti akijikusanyia mahela toka kwa upendo binafsi wa kila mwanachama
Kisha tulipiga picha ya pamoja kwaajili ya kumbukumbu , tulimmiss sana mwenzetu da Rukia alikuwa ametoka kufanyiwa upasuaji muda si mrefu hivyo asingeweza kuja kurukaruka
MC alituongoza kusali sala ya kushukuru kwa mafanikio tuliyopata
No comments:
Post a Comment