hii ndio maana hawa wanawake wenye hekima walichagua vizuri namna ya kuiadhimisha siku ya wanawake ya mwaka 2018, siku ya wanawake ambayo ni tarehe 8 March kila mwaka, mwaka huu iliangukia Alhamis, kwa hekima walizonazo wamama hawa walichagua kuadhimisha siku hiyo kama kikundi mwisho wa wiki yaani jmosi tarehe 10March, ili waweze kujiunga na wanawake wengine siku ya Alhamis ktk kuadhimisha siku hii muhimu kwao. fuatilia matukio hapo chini;
tuliongozwa na Katibu wetu Vesca Lwenje, kushoto na tulipokelewa na Mwalimu mkuu wa shule ya msingi salasala mama
Ngaiza.
Tuliketi ofisini kwa mwalimu mkuu
Mshauri wetu wa Chama Graceana Maganga alitoa historia fupi ya kikundi, na lengo la sisi kutembelea shule hii. Mwenyekiti wetu Eva Bugoye alipata dharura tunasikitika hatukuwa nae siku hii.
Mweka hazina wetu Joyce Swai akipongezana na mwalimu mkuu baada ya kutoa ufafanuzi wa namna fedha za kikundi zinavyo patikana na zinavyotumika
Mwalimu mkuu alikuwa pamoja na msaidizi wake mwalimu William, wote walifurahia ujio wetu na walitupongeza sana kwa moyo tulionao wa kutoa msaada kwa watoto tusowajua
Mzigo wa Madaftari na Pencil HB 621
hope kila mtu anaelewa HB pencil na MOR papers, kwa kifupi ni kwamba siku hizi mtihani wa taifa darasa la saba watoto wanatumia pencil upo hapo!
ni furaha iliyoje tulishusha mzigo na kukabidhi,
sababu iliyotufanya tuchague shule ya msingi salasala ni katika pitapita zetu tuligundua ni miongoni mwa shule dhaifu kwenye wilaya ya kinondoni na ofisi za kikundi chetu zipo jirani na shule Charity begins at home
Mshauri wa chama alimkabidhi Mwalimu mkuu muhtasari wa vifaa vilivyowasilishwa
tulipata pia wasaha wa kusalimiana na watoto wachache wa madarasa mchanganyiko waliokuja kujisomea siku hiyo ya j mosi
nini kilifuata baada ya zoezi la kukabidhi vifaa , stay tuned;
Kazi na dawa, Kazi na sala!''asiyefanya kazi na asile'' baada ya kazi ya kuwasilisha mzigo kwa watoto wetu wamama hatukufanya ajizi siku ya wanawake duniani huja mara moja tu kwa mwaka
tulitafuta kiwanja tulivu na tukajiachia sawasawa, kisha tuka rudi majumbani tukiwa fresh na tayari kwa kuhudumia waume zetu na watoto
I Love HELAU kwa kweli